Yanga imetwaa taji la ligi kuu ya NBC kwa msimu wa nne mfululizo ikiichapa Simba mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Ilikuwa mechi ya upande mmoja kwa muda mwingi katika kipindi cha pili Yanga ikiandikisha ushindi wake kupitia mabao ya Pacome Zouzoua aliyefunga kwa mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari pia akitengeneza bao la pili lililofungwa na Clement Mzize
Ni ushindi unaodhihirisha ubora wa Yanga dhidi ya watani zao Simba na zaidi ni furaha kwa mashabiki wa Yanga kwa kuchukua kombe mbele ya watani zao


