Local,Normal News,Yanga, Singida

Yanga, Singida BS kazi ipo leo, Arajiga kuhukumu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
29 Jun 2025
Yanga, Singida BS kazi ipo leo, Arajiga kuhukumu

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limemteua Ahmed Arajiga, kuwa mwamuzi wa kati wa mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) itakayozikutanisha Yanga na Singida Black Stars leo Jumapili.

Arajiga ni mara ya pili mfululizo kuwa mwamuzi wa kati katika fainali ya michuano hii baada ya kuteuliwa msimu uliopita Yanga ilipoifunga Azam kwa penalti 6-5.

Mbali na hilo, pia Arajiga alichezesha nusu fainali ya Kombe la FA msimu huu, Singida Black Stars ikiichapa Simba kww mabao 3-1, huku akitangazwa kuwa mwamuzi wa kati katika Dabi ya Kariakoo, Yanga dhidi ya Simba iliyotarajiwa kuchezwa Machi 8, 2025 kabla ya kuahirishwa Juni 15, 2025 na kuchezwa Juni 25, 2025 waamuzi kutokea Misri.

Katika fainali itakayochezwa leo Jumapili Juni 29, 2025 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia saa 2:15 usiku, Arajiga atasaidiwa na Frank Komba ambaye pia alikuwa msaidizi wa Arajiga fainali ya msimu uliopita. Hamdani Said pia atakuwa msaidizi namba mbili. Mwamuzi wa akiba ni Tatu Malogo.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
9m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
38m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’