Local,Transfer News,Simba

Simba yajipanga kumuongeza mkataba Fadlu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
30 Jun 2025
Simba yajipanga kumuongeza mkataba Fadlu

Klabu ya Simba SC iko katika hatua za mwisho za mazungumzo na Kocha Mkuu wao, Fadlu Davids, kuhusu kuhuisha mkataba wake ambao umemalizika rasmi.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zimeeleza kuwa tayari Fadlu amekutana na viongozi wa juu wa Simba SC kukamilisha mazungumzo kwa ajili ya kuongeza muda wa mkataba wake.

Hatua hii imechochewa na kazi nzuri aliyoifanya msimu huu, ambapo Simba imeonyesha kiwango bora uwanjani licha ya kuwa hakufanikiwa kushinda taji lolote.

Rais wa heshima wa klabu hiyo, Bilionea Mohammed Dewji β€˜Mo’, ameripotiwa kumhakikishia Fadlu mkataba mpya, kama ishara ya kuthamini mchango wake na kuendelea na mpango wa muda mrefu wa maendeleo ya timu.

Kwa mujibu wa taarifa, Fadlu tayari amewasilisha mapendekezo yake kwa uongozi wa klabu β€” ikiwa ni pamoja na maboresho kadhaa kwenye upande wa kikosi. Hii ni sehemu ya masharti aliyoweka ili kuendelea na kazi Simba.

Mapendekezo hayo yanahusisha usajili mpya pamoja na kuboresha baadhi ya maeneo ya kikosi yaliyobainika kuwa na changamoto msimu uliomalizika.

Akizungumza mara baada ya mchezo dhidi ya watani wa jadi Yanga, Fadlu alisema:

β€œNitawasilisha mapendekezo yangu kwa uongozi, tutaona wao wanasemaje. Kama kile wanachohitaji kiko sawa na ninachohitaji, basi tutasonga mbele,” alisema

Fadlu alijiunga na Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja ambao sasa umefikia mwisho. Mazungumzo ya mkataba mpya yanahusisha pia benchi lake lote la ufundi alilokuja nalo, ambalo linajumuisha watu wengine kama Kocha Msaidizi, Kocha wa Viungo, pamoja na mchambuzi wa video (Video Analyst).

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
6m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
35m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’