Klabu ya Simba SC ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha dili la kumuongeza mkataba nahodha na beki wa kushoto wa muda mrefu, Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr', ambaye amekuwa nguzo muhimu kwenye kikosi cha wekundu wa Msimbazi kwa misimu kadhaa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba, makubaliano kati ya mchezaji huyo na klabu tayari yamefikiwa, na kilichosalia ni utiaji saini rasmi wa mkataba mpya.
Inaripotiwa kuwa Zimbwe Jr aliomba asaini mkataba mpya baada ya msimu wa 2024/25 kukamilika, jambo ambalo uongozi wa Simba umeliridhia.
Zimbwe Jr, ambaye ni miongoni mwa wachezaji waandamizi na wanaoheshimika ndani ya kikosi hicho, anatarajiwa kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili zaidi.
βMakubaliano yapo tayari, Zimbwe alionyesha nia ya kubaki na tunathamini mchango wake kwenye timu,β chanzo kutoka ndani ya Simba kilieleza.
Baada ya kukamilika kwa msimu, Simba SC imeanza rasmi mchakato wa kufanya maboresho ya kikosi chake, ambapo hatua ya kwanza ni kuhakikisha wachezaji waliopendekezwa na benchi la ufundi kuendelea wanapewa mikataba mipya kabla ya usajili mpya kuanza.
Zoezi hili ni sehemu ya mpango wa Simba kurejea katika ubora wake, baada ya msimu uliopita kuishuhudia timu hiyo ikikosa mataji ya ndani na pia kukosa taji la Shirikisho (CAF CC)