Rais wa heshima na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' jana aliongoza kikao cha Bodi kufanya tathmini ya msimu uliopita na kuweka mikakati ya maboresho kuelekea msimu ujao wa mashindano 2025/26
Katika hicho, Bodi ilipata nafasi ya kupitia na kujadili ripoti iliyowasilishwa na Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids ambayo ina mapendekezo yanayohitajika katika kukiboresha kikosi ili kuwa na ushindani zaidi na kushinda mataji msimu ujao
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema kikao hicho ni dalili njema ya mambo mazuri kuelekea maandalizi ya msimu ujao
Ahmed amewataka mashabiki na wanachama wa Simba kuendelea kuwa watulivu wakati mikakati kabambe ikiandaliwa
"Kikao baina ya Bodi ya Wakurugenzi na Baraza la Washauri la klabu yetu ni dalili njema za maandalizi ya msimu ujao. Kwa sasa Wana Simba tuwe watulivu tuwape nafasi viongozi wetu waendeleee na mikakati ya kuitengeneza Simba yetu kwa msimu ujao," alisema Ahmed
Baada ya kikao hicho ni wazi kitakachofuata ni michakato ya maboresho ya kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi kuelekea msimu ujao