Kocha Miguel Gamondi raia wa Argentina amejiunga na Singida Black Stars kuwa Kocha Mkuu akisaini mkataba wa mwaka mmoja
Taarifa ya Singida BS, zimethibitisha tayari kocha huyo wa zamani wa Yanga amesaini mkataba wa kuinoa Singida BS
Anatarajiwa kutua nchini Julai 22 tayari kwa maandalizi ya msimu mpya 2025/26. Singida BS inatarajiwa kuanza rasmi pre-season Julai 25
Wakati akiinoa Yanga, Gamondi aliiwezesha kutwaa taji la Ligi Kuu, Ngao ya Jamii na kombe la CRDB huku pia akiiwezesha Yanga kucheza robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika