Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Julai 04 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Jul 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Julai 04 2025

Newcastle imewasilisha ofa iliyoboreshwa ya pauni milioni 55 kwa winga wa Uswidi Anthony Elanga, 23, na iko mbioni kukubaliana na Nottingham Forest. (Mail)

Real Madrid na kocha Xabi Alonso wamefikia makubaliano ya kuuzwa kwa mshambuliaji wa Brazil Rodrygo, ambaye amekuwa akihusishwa na Arsenal, ikiwa ofa stahiki itatolewa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Athletic - usajili unahitajika)

Fenerbahce imewasilisha ofa ya euro milioni 15 (Β£12.9m) kwa mshambuliaji wa Paris St-Germain Marco Asensio lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anasubiri chaguzi nyingine kutokea, huku klabu za AC Milan na Villarreal zikimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Como wamekubali ofa ya awali ya Β£16.5m kwa winga wa Celtic Mjerumani Nicolas Kuhn, 25. (Sky Sports)

Rangers iko mbioni kukamilisha dili la kiungo wa Luton Town na Norway Thelo Aasgaard, 23. (Daily Record)

Tottenham Hotspur na Chelsea ni miongoni mwa klabu zinazomwinda kiungo wa AZ Alkmaar Mholanzi Kees Smit, 19. (TBR Football)

Al-Nassr huenda ikaelekeza darubini yake kwa winga wa Arsenal Mbrazili Gabriel Martinelli, 24, baada ya kushindwa kumsajili - mshambuliaji wa Liverpool na Colombia Luis Diaz, 28 amabye alikuwa lengo lao kuu. (GiveMesport)

Beki wa Inter Milan na Uholanzi Denzel Dumfries, 29, ana kipengele cha kutolewa cha euro 25m (Β£21.5m) katika kandarasi yake ambayo itatumika hadi katikati ya Julai na inaweza tu kuzingatiwa na klabu isiyo ya Italia. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Mchezaji wa kimataifa wa Ureno Antonio Silva, 21, amekataa ombi la kuhamia klabu ya Al-Hilal ya Saudia, lakini beki huyo wa kati bado anatarajiwa kuondoka Benfica. (A Bola - kwa Kireno) Arsenal wamempoteza meneja wao wa chini ya miaka 21 Mehmet Ali aliyeamua kujiunga na Brentford. (Football London)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
12m ago
READ MORE β†’
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
24m ago
READ MORE β†’
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
1h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
2h ago
READ MORE β†’
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
15h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
17h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
18h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
18h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
19h ago
READ MORE β†’