Local,Normal News,Kagera

Kagera Sugar yaachana na CEO

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Jul 2025
Kagera Sugar yaachana na CEO

Klabu ya Kagera Sugar imetangaza kutokumuongezea mkataba aliyekuwa Mtendaji Mkuu Thabit Kandoro

Taarifa iliyotolewa na Kagera Sugar, imemtakia kila la kheri Kandoro ambaye anaondoka baada ya timu hiyo kushuka daraja

"Uongozi wa Kagera Sugar Football Club unapenda kuutarifu Umma, mashabiki wetu, wanamichezo, na wadau wote wa michezo kuwa klabu imefikia makubaliano rasmi ya kutomuongeza mkataba mpya Mtendaji Mkuu wa Klabu THABITY KANDORO baada ya mkataba wake wa awali kufikia ukomo mwishoni mwa msimu huu wa NBCPL 2024/2025.

Uamuzi huu umefikiwa kwa maelewano na heshima kubwa kati ya pande zote mbili, huku klabu ikimshukuru sana kwa mchango wake mkubwa katika kipindi chote alichoitumikia klabu.

Uongozi unamtakia kila la heri katika majukumu yake mapya ya baadae. Tunaahidi kuendelea kuimarisha mifumo ya kiutendaji ndani ya klabu na tutatoa taarifa rasmi kuhusu mchakato wa kumpata mrithi wake katika muda muafaka.

Tunawaomba mashabiki wetu waendelee kutuunga mkono Katika kipindi hiki ambacho tunafanya maboresho ya kikosi pamoja na Benchi la ufundi kuelekea msimu mpya wa NBC CHAMPIONSHIP 2025/2026."

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’