CAF yatangaza kalenda ya mashindano 2025/26

Joel JJ By Joel JJ β€’ 7th July 2025


CAF yatangaza kalenda ya mashindano 2025/26

Kuelekea msimu mpya wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na kombe la Shirikisho, Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) tayari limetangaza rasmi kuwa mashindano hayo kwa msimu wa 2025/26 yataanza mwezi Septemba.

Mabadiliko haya ya ratiba yamesababishwa na kuandaliwa kwa mashindano ya CHAN yatakayofanyika mwezi Agosti nchi za Kenya, Uganda na Tanzania

Yanga wakiwa mabingwa wa ligi kuu ya NBC wataiwakilisha Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa sambamba na Simba iliyomaliza katika nafasi ya pili wakati Azam Fc na Singida BS wakishiriki kombe la Shirikisho

Habari njema kwa klabu ya Simba ni kuwa haitashiriki raundi ya kwanza ya michuano hiyo ikiwa miongoni mwa vigogo watano Afrika waliokusanya alama nyingi katika kpindi cha miaka mitano

Hatua ya Awali ya Kwanza:

  • Mchezo wa kwanza: Septemba 19–21, 2025

  • Mchezo wa marudiano: Septemba 26–28, 2025

Hatua ya Awali ya Pili:

  • Mchezo wa kwanza: Oktoba 17–19, 2025

  • Mchezo wa marudiano: Oktoba 24–26, 2025

Mechi za Maundi:

  • Siku ya mechi 1: Novemba 21–23, 2025

  • Siku ya mechi 2: Novemba 28–30, 2025

  • Siku ya mechi 3: Januari 23–25, 2026

  • Siku ya mechi 4: Januari 30–Februari 1, 2026

  • Siku ya mechi 5: Februari 6–8, 2026

  • Siku ya mechi 6: Februari 13–15, 2026

Hatua ya Mtoano (Knockout):
Robo Fainali:

  • Mchezo wa kwanza: Machi 13–15, 2026

  • Mchezo wa marudiano: Machi 20–22, 2026

Nusu Fainali:

  • Mchezo wa kwanza: Aprili 10–12, 2026

  • Mchezo wa marudiano: Aprili 17–19, 2026

Fainali:

  • Imepangwa kuchezwa kati ya Mei 8 na 24, 2026

Vipindi vya Usajili wa Wachezaji:

CAF pia imethibitisha dirisha la usajili kwa vilabu vitakavyoshiriki:

  • Usajili wa Hatua ya Awali: Agosti 1–31, 2025

  • Usajili wa Hatua ya Awali ya Pili: Septemba 1–30, 2025

  • Usajili wa Hatua ya Makundi: Oktoba 1–31, 2025

  • Usajili wa Hatua ya Mtoano: Januari 1–31, 2026


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.