Local,Normal News,Simba,Transfer News

Camara mguuni ndani, nje Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Jul 2025
Camara mguuni ndani, nje Simba

Mabosi wa Simba wako sokoni kutafuta golikipa mwingine wa Kimataifa na endapo kama wafanikiwa katika mpango wake, ni wazi golikipa wake namba moja Moussa Camara hatma yake itakuwa shakani

Kuanzia msimu ujao mabadiliko ya kanuni hayataruhusu klabu kuwa na zaidi ya golikipa mmoja wa kigeni

Licha ya kuibuka na tuzo ya golikipa bora wa ligi kuu ya NBC msimu uliomalizika baada ya kukusanya cleanshet 19 akiifikia rekodi iliyowahi kuekwa na Aishi Manula msimu wa 2017/18, Camara anaweza kuponzwa na makosa aliyofanya kwenye mechi chache ambazo kama Simba ingepata matokeo mazuri, basi leo hadithi zingekuwa tofauti

Camara ambaye alitua Simba mwanzoni mwa 2024-2025 akitokea Horoya ya Guinea, amekuwa kipa namba moja kikosini baada ya Ayoub Lakred kuwa na majeraha ya muda mrefu na kuondolewa kwenye usajili wa msimu uliopita

Licha ya kuonyesha kiwango bora, lakini kuna makosa aliyofanya katika baadhi ya mechi za ligi na hata mechi za Kimataifa

Camara alicheza mechi zote za kimataifa za Simba ikicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kupoteza mbele ya RS Berkane ya Morocco.

Katika ligi Camara amecheza mechi 28 kwa dakika 2,520 kati ya mechi 30, ndiye ameibuka kinara wa clean sheet akimaliza na 19, huku akiruhusu mabao 13.

Miongoni mwa makosa aliyofanya yaliyoigharimu Simba ni mechi mbili za ligi dhidi ya Yanga Oktoba 19, 2024 mpira wa faulo uliopigwa na Clatous Chama dakika ya 86 ukionekana kwenda nje aliufuata na kujikuta anaurudisha ndani Maxi Nzengeli akaupiga haraka Kelvin Kijili akajifunga, likawa bao pekee lililoipa Yanga ushindi wa 1-0.

Pia Juni 25, 2025 alitoka golini na kwenda kumfanyia faulo Pacome Zouzoua Simba ikaruhusu bao la kwanza na kupoteza kwa mabao 2-0.

Kabla ya hapo, katika sare ya 2-2 dhidi ya Coastal Union, Oktoba 4, 2024 alifanya makosa mawili yaliyozaa mabao wakati Simba ikiwa mbele kwa 2-0 na mwisho mchezo ukaisha sare ya 2-2.

Baada ya kikao cha Bodi kilichofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni, Simba imeidhinisha kusaka mlinda lango mwingine mwenye sifa na vigezo vilivyoidhinishwa na benchi la ufundi, lakini kama hawatampata basi Camara atanusurika

Lakini ni wazi Camara atahitaji kufanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyoonekana ili kuhakikisha anaipa uhakika Simba katika malengo ya kuwania mataji

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
7m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
36m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’