Local,Transfer News,Simba, Azam

Simba imepania kumsajili Feisal

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Jul 2025
Simba imepania kumsajili Feisal

Mashabiki wa Simba SC wamejaa hamasa. Kwa miezi kadhaa sasa, uvumi umeenea kwamba kiungo nyota wa Azam FC, Feisal Salum, yupo mbioni kujiunga na mabingwa hao wa zamani wa Tanzania katika dirisha hili la usajili la Julai na dili linaonekana kuwa karibu kutimia.

Feisal ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu, kwa sasa anatizamwa kama kiungo bora katika eneo la ushambuliaji msimu uliomalizika akiwa kinara wa kutoa pasi za mabao (13) wakati msimu mmoja nyuma alipachika mabao 19 na pasi nane za mabao

Simba wamehusishwa na Fei Toto tangu mwishoni mwa mwaka 2024, taarifa kutoka ndani ya uongozi imethibitisha Wekundu hao wa Msimbazi tayari wana makubaliano binafsi na Fei Toto kilichobaki ni utaratibu wa kumalizana na Azam Fc

Fei Toto bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Azam Fc ambao utamalizika Juni 2026. Kuna taarifa kuwa Azam Fc wana makubaliano na klabu yake ya zamani Yanga kuwa endapo Azam Fc itamuuza ndani ya nchi itapaswa kulipa Tsh Bilioni 1 kwa Yanga

Licha ya Kaizer Chiefs kuwasilisha ofa kwa Azam Fc kutaka kumnunua, fundi huyo kutoka Zanzibar ameweka ngumu akisubiri uhamisho wake kuelekea Msimbazi ukamilike

Ni usajili unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Simba SC hasa ikizingatiwa timu yao inasukwa upya kwa ajili ya msimu ujao wa mafanikio baada ya kwenda misimu minne bila kushinda mataji makubwa

Kwa sasa mitandaoni mashabiki wa Simba wanawasukuma viongozi wao kuharakisha kukamilisha usajili huo kwani zipo taarifa waajiri wake wa zamani Yanga wanamshawishi arejee katika klabu hiyo licha ya mvutano uliojitokeza baina yao wakati Feisal anataka kujiunga na Azam Fc

Katika moja ya mahojiano yake, Mfadhili wa zamani wa Simba Azim Dewji ambaye ni baba mdogo wa mwekezaji wa Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo', alidokeza kuwa Fei Toto msimu ujao atacheza Simba

"Kuna mambo fulani fulani yanawekwa sawa lakini naamini kila kitu kitakamilika na Fei atacheza Simba msimu ujao," alisema

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’