Local,Normal News,Dodoma, Tabora

Dodoma Jiji kumshusha kocha Mcongo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Jul 2025
Dodoma Jiji kumshusha kocha Mcongo

Mabosi wa Dodoma Jiji FC wako katika mazungumzo ya kuipata saini ya aliyekuwa kocha wa Tabora United, Mkongomani Anicet Kiazayidi baada ya kuvutiwa na uwezo wake, wakiamini atatengeneza kikosi bora kitakacholeta ushindani mkubwa msimu ujao.

Taarifa za uhakika zinaeleza kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, Mecky Maxime aliyejiunga na timu hiyo, Juni 19, 2024, akitokea Ihefu ambayo kwa sasa ni Singida Black Stars, huenda akaachana na kikosi hicho licha ya mkataba alionao.

Chanzo kutoka ndani ya timu hiyo, kimeeleza kuwa Maxime amebakisha mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuiongoza kwa msimu ujao, ingawa huenda akaondoka kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na mabosi wake kwa siku za hivi karibuni.

β€œAmekuwa na maelewano mabaya na viongozi wa juu na yeye mwenyewe amejishtukia akiamini huenda akaondoka kutokana na hali iliyopo, hadi sasa hakuna muafaka uliofikiwa kwa sababu ana mkataba pia wa mwaka mmoja uliobaki,” kilisema chanzo hicho.

Akizungumzia juu ya taarifa hizo, Katibu Mkuu wa Dodoma Jiji, Fortunatus Johnson alisema anachotambua Maxime ana mkataba wa mwaka mmoja uliobakia, hivyo kuhusu mambo mengine ya kuondoka kwake bado hakuna kilichofanyika baina ya pande mbili.

β€œTangu tumemaliza Ligi Kuu msimu huu wa 2024-2025, Juni 25, 2025, tunatarajia kufanya kikao chetu Julai 10, kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya kuboresha timu yetu, hivyo hayo ndiyo ninaweza kuyazungumzia kwa sasa,” alisema Fortunatus.

Hata hivyo, licha ya kauli ya Fortunatus, Dodoma wamefanya mazungumzo na Anicet kwa ajili ya kuifundisha msimu ujao, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa msimu uliopita alipokuwa anaifundisha Tabora United.

Anicet alijiunga na Tabora Novemba 2, 2024, ili kuchukua nafasi ya Mkenya Francis Kimanzi aliyeondoka Oktoba 21, 2024, ingawa Mkongomani huyo aliondoka Machi 28, 2025, baada ya kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake wa pande mbili.

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
37m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’