Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Kennedy Musonda raia wa Zambia, amejiunga na klabu ya Hapoel Ramat Gan inayoshiriki ligi daraja la kwanza Israel
Musonda amejiunga na timu hiyo akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga
Baada ya miaka miwili na nusu ya mafanikio akiwa na Yanga, Musonda jana aliwaaga mashabiki na wanachama wa Yanga kwa ushirikiano aliopata katika kipindi chote alichoitumikia Yanga
Katika muda wote alioitumikia Yanga, Musonda alifungia mabao 34 na kutoa asisti 13 na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho na robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika