Ibenge aja na mkakati wa kuongeza mashabiki Azam Fc

Joel JJ By Joel JJ
•
8 Jul 2025
Ibenge aja na mkakati wa kuongeza mashabiki Azam Fc

Juzi Azam Fc ilimtambulisha Florent Ibenge (63) kuwa Kocha Mkuu kwa mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongeza kulingana na mafanikio.

Ibenge, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) alikuwa Kocha Mkuu wa Al Hilal ya Sudan, amejiunga Azam akirithi mikoba ya Rachid Taoussi aliyemaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.

Akizungumza wakati wa hafla ya utambulisho wake, Ibenge alisema amefurahi kujiunga na moja ya timu kubwa Tanzania yenye maono ya kufika mbali na kuahidi kutimiza malengo hayo kwa kushirikiana na benchi lake la ufundi.

Alisema anatambua ugumu wa ligi ya Tanzania yenye ushindani unaotawaliwa na Yanga na Simba na kueleza akipata ushirikiano mzuri anaona huu utakuwa wakati wa kuwa na kizazi kitakachoimba Azam.

“Malengo ya Azam ni kuwa timu kubwa yenye ushindani na kutwaa mataji, kwa kushirikiana na uongozi, wachezaji pamoja na mashabiki tunaweza timiza ndoto hiyo”. 

“Wapo waliozaliwa wakaikuta Yanga na Simba na kuzifanya timu hizi kuwa na mashabiki wengi, ni wakati sasa wa kutengeneza historia ya kuwa na kizazi kitakachoipenda Azam, si kwa njia nyingine bali kwa kushinda michezo na kushirikiana na mashabiki waliopo,” alisema

Aidha, Ibenge aliweka wazi kuwa baada ya tathimini atakayofanya wachezaji bora watasalia na wale wasiotosha watapisha ili wengine waje.

Ibenge amewahi kufundisha timu ya taifa ya DRC mwaka 2014 hadi 2019, vilevile AS Vita (DRC) 2012-2021, RS Berkane (Morocco) 2021-2022 pamoja na Al Hilal (Sudan) 2022-2025.

Miongoni mwa mafanikio ni kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN 2016) akiwa kocha wa timu ya taifa wa DRC. Pia, mwaka 2015 aliifikisha DRC nusu fainali ya Mataifa ya Afrika (AFCON) na kuibuka mshindi wa tatu.

Akiwa na RS Berkane aliibuka bingwa wa Kombe la Shirikisho la Afrika (CAF) mwaka 2022 pia aliiongoza RS Berkane kutwaa Super Cup dhidi ya Wydad Casablanca.

Mwaka 2014 aliifikisha AS Vita fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, akimaliza mshindi wa pili. Hali kadhalika msimu huu aliifikisha Al Hilal hatua ya robo finali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

ADVERTISE HERE

More Stories

Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
4m ago
READ MORE →
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
56m ago
READ MORE →
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE →
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE →
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE →
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE →
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE →
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
9h ago
READ MORE →
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE →
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE →