Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Julai 10 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Jul 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Julai 10 2025

Napoli wamerejea tena kumuwania winga wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho, 21, na wanatumai wanaweza kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kwa pauni milioni 45 (Mirror).

United wanaendelea kuwa na matumaini ya kukubaliana na Brentford na mshambuliaji wa Cameroon Bryan Mbeumo, 25, kwa wakati ili mshambuliaji huyo awe sehemu ya ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya nchini Marekani (Sky Sports).

Mazungumzo ya Arsenal ya kumsajili mshambuliaji wa Sporting na Sweden Viktor Gyokeres, 27, yanasuasuakutokana na tofauti ya maoni kuhusu thamani na masharti ya jumla (Independent). Newcastle United wamekataa ofa ya tatu kutoka Leeds United kwa kiungo wa Kiingereza Sean Longstaff, 27 (Northern Echo).

Al-Hilal wanamtaka mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 22, ambaye pia anasakwa na Arsenal. Klabu hiyo ya Saudi Pro League pia inavutiwa na mshambuliaji wa Ufaransa wa Crystal Palace, Jean-Philippe Mateta, 28 (Sun).

Aston Villa na Brighton wanamfuatilia kiungo mshambuliaji mwenye kipaji kikubwa kutoka Benin, Rodolfo Aloko, 18, anayetoka klabu ya Kroatia NK Kustosija (Mail).

Manchester United wanatarajia kumuuza winga wa Kiingereza Jadon Sancho, 25, kwa ada ya uhamisho iliyopunguzwa kwa kiasi kikubwa (Givemesport).

Nottingham Forest na Crystal Palace ni miongoni mwa vilabu vya Ligi Kuu vinavyomfuatilia kiungo wa Manchester City na England wa timu ya taifa ya vijana ya U-21s, James McAtee, 22, msimu huu wa joto (Sky Sports).

Liverpool wanaweza kujiunga na Arsenal katika mbio za kumsajili winga wa Real Madrid na Brazil Rodrygo, 24, ikiwa wataishia kumpoteza winga wa Colombia Luis Diaz, 28, kwa Barcelona (Sacha Tavolieri via Goal).

Winga wa Ureno Chiquinho, 25, ameondoka Wolves kujiunga na Alverca nchini Ureno kwa mkataba wa kudumu, huku klabu hiyo ya Ligi Kuu ikibaki na kipengele cha asilimia 40 cha mauzo ya baadaye (Fabrizio Romano).

Brighton wako tayari kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson kwenda Roma lakini klabu hiyo bado haijapata idhini kutoka kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 (Calciomercato).

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
1h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
1h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
2h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
3h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
4h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
6h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
8h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
9h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
10h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
11h ago
READ MORE β†’