Local,Transfer News,Azam, Hilal

Ibenge kuvuta beki Al Hilal

Joel JJ By Joel JJ
β€’
14 Jul 2025
Ibenge kuvuta beki Al Hilal

Azam Fc imeanza mazungumzo na Al Hilal ya Sudan ili kupata saini ya beki wa kulia, mkongomani Steven Ebuela, ambaye yuko nchini kwa takriban wiki sasa.

Azam imeanza maandalizi mapema ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2025/26, ikiwatambulisha baadhi ya wachezaji wake akiwemo kipa Aishi Manula, Muhsin Malima, Lameck Lawi na Kocha Florent Ibenge.

Sasa timu hiyo imeanza mazungumzo na Al Hilal ili kumnunua beki wa kulia, Ebuela. Nyota huyo bado ana mkataba na mabingwa hao wa Sudan hadi Juni 30, 2027, alijiunga nao mwaka 2023 akitokea AS Maniema ya nchini kwao Congo.

Majibu waliopewa viongozi wa Azam baada ya mazungumzo ya awali ni ili kumwachia mlinzi huyo, wanapaswa kutoa zaidi ya Sh300 milioni.

"Ni chaguo la Kocha Ibenge, amependekeza kuongezewa beki huyo ambaye aliwahi kufanya naye kazi. Sasa mazungumzo bado yanaendelea kwa sababu bado ni mchezaji wa Al Hilal," kilisema chanzo.

Kama Ebuela atasaini Azam, atakwenda kwenye eneo la beki wa kulia ambalo kwa sasa linashikiliwa na nahodha wa timu hiyo, Lusajo Mwaikenda, ambaye amekuwa na msimu bora akifunga mabao sita Ligi Kuu.

Akiwa na Al Hilal, Ebuela alicheza mechi zote za Ligi ya Mabingwa Afrika akianza ya makundi dhidi ya Yanga kwa dakika zote 90, kijumla kacheza dakika 720 kwenye mechi nane.

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’