Rais wa heshima wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' amesema ametenga fedha za kutosha kwa ajili ya usajili ili kuhakikisha kikosi cha Simba kinafanyiwa maboresho muhimu ili kufanya vyema zaidi msimu ujao
Mo alitoa kauli hiyo jana katika tamko maalum alilotoa kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii
Aidha Mo amewataka Wanasimb kuwa wamoja katika kupigania malengo ya Simba ambayo ni kushinda mataji na kuwa klabu namba moja barani Afrika
"Tutaongeza nguvu kwenye benchi la ufundi ili kuhakikisha timu yetu inapata muongozo sahihi kwa kufikia mafanikio"
"Pia tutaimarisha bodi ya Wakurugenzi, Kamati za ndani na mifumo ya kitaasisi ili kuhakikisha mafanikio ni ya kudumua"
"Nimetenga fedha za kutosha kuhakikisha timu yetu inakuwa bora zaidi na kwa mema ya Mwenye ez Mungu Simba itajulikana kwa makubwa zaidi"
"Ndugu zangu Wanasimba, nimewekeza muda wangu, nimewekeza jasho, damu na fedha katika Simba. Sio kwa sababu nyingine, bali kwa mapenzi ya dhati kwa klabu hii na kwa Taifa letu"
"Ninawaomba tusimame pamoja, tuendelee kuamini, kushirikiana na kulinda heshima ya klabu ya Simba, naahidi sitaacha kuipigania Simba ndoto yangu haijabadilika Simba kuwa klabu namba moja barani Afrika kwa uwezo wa Mwenye ez Mungu," alisema Mo
Katika hatua nyingine Mo, amewajibu wale wenye mashaka na uwekezaji wake Simba akibainisha kuwa tangu mwaka 2017, ametumia takribani Tsh Bilioni 87 kuwekeza ndani ya Simba
"Nimeweka Tsh Bilioni 45 kwa ajili ya mshahara, usajili na matumizi mengine ya klabu. Pia nimechangia Tsh Biilioni 20 kama sehemu ya ununuzi wa hisa asilimia 49 ndani ya Simba Sc. Na mara nyingi nimekuwa nikitoa msaada nje ya mfumo rasmi kila palipojitokeza uhitaji wa dharura kuanzia mwaka 2017 hadi mwaka 2024 nimetumia takribani Bilioni 22 katika misaada ya dharura na hivyo kufanya jumla ya mchango wangu kwa Simba kufikia Bilioni 87"
"Kusema Mo hatoi hela ni kauli ya kupotosha yenye muelekeo wa chuki, tuachane na fitna zisizo na msingi, tujenge palipotoboka, tuzibe ufa panapovuja na tusonge mbele bila ya kuonyeshana vidole"