International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne, Julai 15 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Jul 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne, Julai 15 2025

Arsenal inajiandaa kuwasiliana na Crystal Palace kujadili iwapo inaweza kumsajili winga wa Uingereza Eberechi Eze bila kuanzisha kipengele cha kutolewa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa pauni milioni 68. (Sportsport)

Liverpool imefanya mazungumzo na mshambuliaji wa Crystal Palace Jean-Philippe Mateta, 28. Mfaransa huyo amekutana na wawakilishi wa klabu hiyo mjini Paris. (Footmercato - kwa Kifaransa)

Manchester United imefikia makubaliano na Brentford kumsajili mshambuliaji wa Cameroon Bryan Mbeumo, 25. (UFootball Transfers)

Brentford inafikiria kumsajili winga wa Ipswich Town na England aliye na umri wa miaka 21 Omari Hutchinson kama mbadala wa Mbuemo. (Standard)

Wakala wa Joao Felix amekuwa akisaidia katika mazungumzo ya mshambulizi wa Chelsea mwenye umri wa miaka 25 kuhamia Benfica. (A Bola - kwa Kireno)

Chelsea inavutiwa sana na winga wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho, 21, baada ya kufanya mazungumzo ya awali mwezi Januari, (TBR Football)

West Ham imewaongeza wachezaji wawili wa Liverpool walio chini ya umri wa miaka 21, mshambuliaji Harvey Elliott, 22, na kiungo mkabaji Tyler Morton, 22, kwenye orodha ya walengwa. (Mail)

Manchester United imewasiliana na klabu ya Lyon kuhusu kiungo wa kati wa Ufaransa Corentin Tolisso, 30. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, 36, anatarajiwa kuondoka Al-Qadsiah ya Saudi Arabia na kujiunga na klabu ya Ufaransa ya Marseille. (La Provence - kwa Kifaransa)

Manchester City itamuuza kiungo wa kati wa England chini ya umri wa miaka 21 James McAtee, 22, msimu huu wa kiangazi kwa lengo la kunufaika kutokana na Kanuni za Faida na Uendelevu (PSR) na sheria zinazodhibiti matumizi ya klabu (FFP). (Football Insider)

McAtee yuko nchini Ujerumani kutembelea Eintracht Frankfurt kama sehemu ya mpango wa klabu amabayo huenda akajiunga nayo. (Fabrizio Romano)

Wolves inakaribia kufikia mkataba wa pauni milioni 15 kwa winga wa Fluminense na Colombia Jhon Arias, 27. (Mail)

Kiungo wa kati wa Uswizi Granit Xhaka amekubali kujiunga na klabu ya Saudi Pro Neom SC, ambayo bado haijakamilisha ada na Bayer Leverkusen kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32. (Sky Sports Ujerumani)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
48m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’