Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza maombi ya Leseni za Klabu msimu wa 2025/2026 kwa Ligi Kuu ya NBC, Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) yamefunguliwa kwa njia ya mtandao (Online) kuanzia Julai 14, 2025.
Mwisho wa kuwasilisha maombi kupitia mtandao https://clop.cafonline.com itakuwa Agosti 15, 2025.
TFF imezitaka kuhakikisha nyaraka na taarifa zote zinawasilishwa kwa wakati, hakutakuwa na muda wa ziada baada ya dirisha la maombi kufungwa.
Aidha klabu yoyote itakayokuwa inadaiwa na mchezaji haitapatiwa leseni ya kushiriki Ligi na kwa Klabu itakayoshiriki mashindano ya CAF, Kocha Mkuu ni lazima awe na Diploma A ya CAF na Kocha Msaidizi awe na Diploma B ya CAF.
