Local,Transfer News,Yanga, Simba

Beki wa zamani Simba apewa Thank You FAR Rabat

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Jul 2025
Beki wa zamani Simba apewa Thank You FAR Rabat

Klabu ya FAR Rabat imemalizana na beki wake Henock Inonga 'Varane' baada ya msimu mmoja ndani ya timu hiyo.

Inonga aliyetambulishwa ndani ya FAR Rabat Julai 13, 2024, amesitishiwa mkataba, kutokana na ripoti ya kocha Mreno Alexander Santos.

Beki huyo wa zamani wa Simba, hakuwa na maisha mazuri ndani ya timu hiyo, akianza kwenye mechi tano pekee msimu huu, zikiwemo nne za Ligi na Moja ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Inonga amekuwa akisotea benchi ndani ya FAR Rabat huku mechi nyingi akiwa anakaa jukwaani

Β Mapema Santos alionyesha hakubaliani na uwezo wake, ambapo aliwajulisha mabosi wa timu hiyo ya jeshi la Mfalme, kuachana na beki huyo Januari, 2025.

Inonga ameachwa sambamba na nyota wengine wanne wakiwemo, Hicham Boussefiane,El Hassan Houbeib,Et-Tayeb Boukheriss na Larbi Naji.

Beki huyo Mkongomani aliwahi kutajwa kupigiwa hesabu na Yanga wakati ikisaka beki wa kati lakini ni kama wameachana na mpango wa kumsajili.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’