Local,Transfer News,Yanga

Kocha Mpya wa Yanga ni huyu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Jul 2025
Kocha Mpya wa Yanga ni huyu

Baada ya tetesi zilizoenea kwa wiki kadhaa, hatimaye ukweli umefahamika, aliyekuwa kocha msaidizi wa Mamelodi Sundowns, Romain Folz, yupo mbioni kutangazwa rasmi kama kocha mkuu mpya wa klabu ya Yanga.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 35 anarudi katika soka la CAF Champions League kupitia dili hili kubwa na vigogo hao wa soka Afrika Mashariki waliomaliza msimu wa 2024/25 wakiwa na mataji yote ya ndani.

Inaelezwa kuwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Hersi Ally Said, alipata mapendekezo ya nguvu ya kumuajiri kocha huyo raia wa Ufaransa kutoka kwa Arsène Wenger, Mkuu wa Maendeleo ya Soka Duniani ndani ya FIFA walipokutana kwenye Kombe la Dunia la Klabu hivi karibuni.

Vyanzo vya ndani ya klabu vimebainisha kuwa Folz tayari yuko nchini na huenda akatambulishwa wiki ijayo kuchukua rasmi nafasi ya Miloud Hamdi aliyejiunga na klabu ya Ismaily ya Ligi Kuu ya Misri.

Folz anakuja Yanga akiwa na historia ya aina yake akizitumikia klabu mbalimbali na hata timu za Taifa katika majukumu ya Kocha Mkuu, Kocha Msaidizi au Mkurugenzi wa ufundi

Alimaliza msimu uliopita akiwa na Olympique Akbou ya Algeria ambapo aliisaidia klabu hiyo kubaki ligi kuu katika mechi nane za mwisho. Pia amewahi kupitia klabu kama Township Rollers, Marumo Gallants, AmaZulu na Horoya AC.

Kwa kujiunga na Yanga, Folz anafungua ukurasa mpya katika safari yake ya ukufunzi, safari inayotarajiwa kuwa ya changamoto lakini yenye matarajio makubwa, hasa katika kuhakikisha Yanga SC inasalia kuwa nguvu ya kutisha kwenye soka la Afrika.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
37m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’