Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amewataka mashabiki wa timu hiyo kusubiri taarifa rasmi ya uongozi kuhusu hatma ya nahodha wa timu hiyo Mohammed Hussein 'Tshabalala'
Ahmed amekiri Zimbwe Jr amemaliza mkataba wa kuitumikia Simba na viongozi wamefanya jitihada kumuongezea mkataba mpya
Msemaji huyo wa Wekundu wa Msimbazi, amesema mashabiki wasubiri kile ambacho viongozi watafanya kuhusu mchezaji huyo kwa kuzingatia maslahi mapana ya klabu
"Wanasimba hawapaswi kuwa na taharuki, wanachopaswa ni kutulia kusubiri taarifa rasmi ya klabu. Ni Kweli Mohamed Hussein "Tshabalala" amemaliza mkataba wake ndani ya Simba SC"
"Zipo juhudi ambazo zimewahi kufanyika kwa ajili ya kumbakisha kunako Klabu yetu. Kila mmoja anafahamu umuhimu wake, kila mmoja anafahamu thamani yake na kila mmoja anafahamu historia njema ya Mohamed Hussein pamoja na Simba SC"
"Zipo Juhudi ambazo zimefanyika kumbakisha mchezaji lakini ni lazima wanasimba tuwe tayari kupokea taarifa yoyote ambayo viongozi wetu wataamua kuhusiana na Mohamed Hussein 'Tshabalala', " Ahmed aliiambia eFM redio
Tetesi zinamuhusisha Tshabalala kutua klabu ya Yanga baada ya mkataba wake na Simba kufikia tamati