Local,Transfer News,Yanga

Aucho agoma kuongeza mkataba Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Jul 2025
Aucho agoma kuongeza mkataba Yanga

Kiungo wa Yanga Khalid Aucho huenda asiwe sehemu ya kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria msimu ujao baada ya majadiliano ya kuhuisha mkataba wake kutofikia mwafaka, imefahamika

Yanga ilikuwa tayari kumpa Aucho mkataba wa mwaka mmoja lakini kiungo huyo hayuko tayari kuongeza mwaka mmoja, akihitaji mkataba wa miaka miwili

Mtu wa karibu wa Aucho ambaye ni mwanahabari, amesema Aucho huenda akaelekea Vietnam alikopata ofa nono zaidi

"Baada ya kikao cha wiki nzima, mimi kama Mwanahabari niliyekuwa na nafasi ya kuyaongea kutoka kwake na uongozi wa Yanga, rasmi Aucho hatokuwa na Yanga"

"Aucho anaweza kwenda Vietnam, kuna klabu ya Ligi Kuu ya huko imemuhitaji, naweza kusema Aucho hatakuwepo nchini msimu ujao," alisema Justine Kessy

Awali Yanga ilikuwa na makubaliano na Aucho kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja lakini huenda fundi huyo kutoka Jinja akawa amebadili mawazo baada ya kushawishiwa na ofa kutoka nje

Katika eneo analocheza Aucho, Yanga tayari imemsajili kiungo Mohamed Doumbia huku pia ikihusishwa kukamilisha usajili wa kiungo kutoka CS Sfaxien Moussa Balla Conte

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’