Local,Transfer News,

Yanga inashusha vifaa sasa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Jul 2025
Yanga inashusha vifaa sasa

Jana Yanga ilitambulisha usajili wa kwanza katika dirisha hili, kiungo mkabaji Moussa Balla Conte aliyetua kutoka klabu ya CS Sfaxien

Conte alitua nchini mapema jana na kusaini mkataba wa miaka mtatu ambao utamuweka Jangwani hadi Julai 2028

Awali Yanga ilipanga kuanza kutoa taarifa za usajili siku ya Jumapili, Julai 20 lakini sintofahamu iliyogubika usajili wa nyota huyo ilipelekea viongozi wa Yanga kuamu kumaliza utata mapemaa kwani kuna taarifa zilidai nyota huyo amegoma kucheza Yanga licha ya mabingwa hao wa nchi kumalizana na klabu yake

Huo ni usajili wa kwanza kutambulishwa, taarifa za usajili zitafahamika zaidi wiki ijayo ikiwa ni wiki ya mwisho kabla ya taratibu za pre-season kuanza

Juzi wakati akizungumza na chombo kimoja cha habari, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alidokeza kuwa mpaka sasa bado usajili wa mchezaji mmoja tu ili Yanga kufunga hesabu zake za usajili katika dirisha hili

Kwa mujibu wa taarifa za ndani, hawa hapa wachezaji ambao tayari wamemalizana na Yanga;

  • Moussa Balla Conte (DM)
  • Mohamed Doumbia (CM)
  • Offen Chikola (AM)
  • Celestin Ecua (AM)
  • Abdulnasir Mohammed (DM)
  • Β Aboubakar Nidhar Otham (CB)

Kwa mujibu wa taarifa, hizi hapa sajiri zinazosubiri kukamilika;

  • Mohammed Hussein (LB)
  • Feisal Salum (AM)

Aidha inaelezwa kuwa Yanga inaweza kusajili nyota wengine wawili katika nafasi ya beki wa kati na mshambuliaji hasa endapo dili la Clement Mzize kuelekea Zamalek kama litakamilika

Yanga inahusishwa na walinzi wawili raia wa DR Congo, Hennock Inonga ambaye ni mchezaji huru baada ya kumalizana na FAR Rabat na Kevin Mondeko aliyesitisha mkataba wake na USM Alger

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’