Klabu ya Simba imempa mkataba kiungo mshambuliaji Morice Abraham aliyekuwa akifanya majaribio kwa miezi kadhaa
Morice aliyerejea nchini mapema mwaka huu akitokea Serbia baada ya kuachana na FK Spartak ya nchini humo, alijumuishwa katika kikosi cha Simba kama sehemu yake ya majaribio
Inaelezwa Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amependekeza kusajiliwa kwa mchezaji huyo ambaye kwa nyakati tofauti ameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'
Morice anaweza kutumika kama kiungo mshambuliaji namba 10 lakini pia anaweza kucheza kama winga
Fadlu alipata muda wa kutosha kumfanyia tathmini akifanya mazoezi na kikosi cha Simba kwa takribani wiki 10



