Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali ameendelea kusisitiza na kuwataka Wanamsimbazi wawe watulivu wakati uongozi ukikamilisha michakato ya usajili
Ahmed amesema usajili uliofanyika katika dirisha hili ni bora pengine kuliko katika wakati mwingine wowote kwa sababu ni mapendekezo ya benchi la ufundi kwa asilimia 100
"Timu inaendelea na usajili, tunasubiri muda tuanza kuwatangaza, viongozi wetu wametapakaa nchi mbalimbali hapa Afrika kwa ajili ya kumalizana na wachezaji husika ili tuwalete ndani ya klabu yetu"
"Niseme kitu kimoja muhimu, katika miaka mingi ya Simba Sc, huu ndio mwaka ambao tunafanya usajili unaotokana na mapendekezo ya benchi la ufundi kwa asilimia 100"
"Tunafanya usajili kutokana na mapendekezo ambayo yametolewa na Mwalimu Fadlu Davids"
"Safari hii sitakuwa na mambo mengi sana kwenye usajili, nitakuwa nadondosha kidogi kidogo mashine zikitua, nitaacha watu waone wenyewe aina ya mali ambazo tutazishusha," alitamba Ahmed



