Simba iko katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mlinzi wa kushoto Khadim Diaw anayetua kutoka klabu ya Al Hilal
Diaw anachukua nafasi ya Mohammed Hussein aliyeachwa baada ya mchakato wa kumuongezea mkataba kukwama
Diaw sasa anakwenda kuwa chaguo la kwanza katika safu ya ulinzi upande wa kushoto
Khadim Diaw ni miongoni mwa wachezaji muhimu katika kikosi cha Al Hilal akicheza kwa mafanikio makubwa.
Msimu uliopita, alikuwa sehemu ya kikosi kilichofika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, na mchango wake uliisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Mauritania, licha ya kuwa walialikwa kushiriki ligi hiyo.
Huu ni usajili muhimu kuelekea msimu ujao hasa kutokana na uzoefu wake mkubwa katika soka la kimataifa barani Afrika.



