International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Julai 21 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Jul 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Julai 21 2025

Real Madrid wanamfuatilia beki wa Arsenal na Ufaransa William Saliba, 24 (L'Equipe). Bosi wa Manchester United, Ruben Amorim, anataka kusajii wachezaji wawili zaidi katika dirisha hili la usajili (Mirror).

United pia wamepeleka ofa kwa ajili ya mshambuliaji wa Sporting Viktor Gyokeres, 27, na wanatumai wanaweza kumshawishi ajiunge nao na kuiacha Arsenal (A Bola).

Na walikataliwa nia yao ya kumsajili mshambuliaji wa Italia Francesco Pio Esposito, 20, na Inter Milan mnamo Januari (Football Italia).

Mshambuliaji wa Cameroon Bryan Mbeumo, 25, amekamilisha vipimo vyake vya afya kwa Manchester United, na hivyo kutua Old Trafford kutoka Brentford (Fabrizio Romano).

Manchester City wameweka bei ya pauni milioni 35 kwa kiungo wa Kiingereza James McAtee, 22, huku vilabu kama West Ham na Eintracht Frankfurt vikimtaka (Telegraph).

Real Madrid wako tayari kusubiri kumsajili beki wa Ufaransa anayechezea Liverpool Ibrahima Konate, 26, bure msimu ujao wa joto lakini wanaweza kutoa ofa ndogo katika dirisha hili la usajili (Football Insider).

Mkataba nono wa Saudi kwa ajili ya mshambuliaji wa Brazil na Real Madrid Vinicius Jr, 25, umeondolewa mezani kwa sasa, lakini unaweza kurejeshwa tena mwaka 2026 (AS).

Tottenham wako tayari kutoa fedha inayohitajika kwa ajili ya beki wa Ukraine na Bournemouth Illia Zabarnyi, 22 (Caught Offside).

Nottingham Forest inaongoza katika mbio za kumsajili kiungo wa Kiingereza Jacob Ramsey, 24, kutoka Aston Villa (Football Insider). Sunderland wamejiondoa kwenye dili la pauni milioni 17.5 la kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Armand Lauriente, 26, kutoka klabu ya Italia Sassuolo (Northern Echo).

Leeds United wanataka vita ya kumfukuzia mshambuliaji wa Hispania Mateo Joseph, 21, ianze kwa matumaini wanaweza kupata fedha nyingi kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Brazil na Fulham Rodrigo Muniz, 24 (Sun).

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’