Kiungo mahiri Mudathir Yahya bado yupo sana na Wananchi kwani mabingwa hao wa soka Tanzania Bara wamethibitisha ameongeza mkataba wa miaka miwili
Ukizungumzia wachezaji waliokuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Yanga kwenye misimu miwili iliyopita, Mudathir ni mmoja wao
Kulikuwa na majaribio ya hapa na pale kumn'goa Mudathir ambapo klabu ya Simba ilikaribia kumsajili kabla ya Yanga kushitukia mchezo na kumalizana nae haraka
Yanga iliweka wazi malengo yake baada ya msimu kumalizika; kuwaongezea mikataba wachezaji wote waliomaliza mikataba ambao wamependekezwa kuendelea kuwa sehemu ya kikosi
Lakini pia kusajili wachezaji bora ambao wataifanya Yanga iendelee kuishi katika malengo yake ya kushinda mataji
Mpaka sasa tayari Yanga imetambulisha usajili wa kiungo mkabaji Moussa Balla Conte kutoka klabu ya CS Sfaxien



