Local,Transfer News,Singida

Manyama aondoka Singida Black Stars

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Jul 2025
Manyama aondoka Singida Black Stars

Uongozi wa Singida Black Stars umefikia makubaliano ya kuachana na kiraka, Edward Charles Manyama baada ya kuitumikia kwa msimu mmoja.

Manyama alijiunga na Singida BS msimu uliomalizika kwa mkataba wa miaka miwili akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Azam FC.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Singida Black Stars kimethibitisha kuwa uongozi wa timu umefikia makubaliano na nyota huyo ili kupisha usajili mwingine.

β€œNi kweli tumefanya mazungumzo na mchezaji huyo na kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wa mwaka mmoja uliokuwa umebaki ili kupisha usajili wa nyota wengine na kumpa nafasi ya kutafuta changamoto nyingine katika dirisha hili,” alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza;

β€œTunathamini mchango wake kwenye kikosi chetu akiitumikia Singida kwa msimu mmoja sasa tunapambana kuimarisha kikosi ambacho tunatarajia kitakuwa na ushindani ndani na kimataifa baada ya kupata nafasi ya uwakilishi.”

Mbali na Manyama pia Singida imeachana na Habib Kyombo na winga Hamad Majimengi ambao wote walikuwa kwa mkopo nje ya timu hiyo baada ya kumaliza mikopo yao wamefanya mazungumzo ya kumalizana nao.

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
4m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
33m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’