Local,Normal News,Simba

Simba yafunguka mipango ya pre-season

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Jul 2025
Simba yafunguka mipango ya pre-season

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema mipango ya maandalizi ya msimu mpya 'pre-season' inaendelea ambapo klabu itaanza maandalizi ya awali hapa nchini kabla ya kusafiri nje ya nchi

Ahmed amesema mwishoni mwa mwezi huu wachezaji watarejea kambini kwa ajili ya taratibu za awali za maandalizi hayo

"Kwa wachezaji ambao tunaendelea nao nafikiri wao tayari wameanza kurejea, kwa hawa wpya tunatarajia hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu wataripoti kwa ajili ya hatua za awali za maandalizi yetu ya pre-season"

"Nafikiri tutaanzia hapa nchini kabla ya kusafiri nje ya nchi, baadae tutatoa taarifa juu wapi timu itakwenda kuweka kambi," alisema Ahmed

Awali Simba ilipanga kuanza pre-season Ijumaa ya Julai 25, lakini ni kama zoezi hilo limesogezwa mbele kwa siku chache

Habari njema ni kuwa bado kuna muda wa kutosha wa kufanya maandalizi kwani ligi zinatarajiwa kurejea katikati ya mwezi Septemba 2025

Michuano ya CHAN 2024 imepelekea mabadiliko hayo ikifanyika kuanzia August 02 hadi August 30

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
4m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
33m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’