Tetesi za sajili zilizokamilika Msimbazi

Joel JJ By Joel JJ β€’ 24th July 2025


Tetesi za sajili zilizokamilika Msimbazi

Mpaka sasa inaelezwa Simba imekamilisha usajili wa nyota watano wa kigeni katika mkakati wa kukiboresha kikosi cha Simba kuelekea mikiki mikiki ya michuano mbalimbali msimu ujao

Katika orodha hiyo kuna mawinga wawili, beki wa kushoto, kiungo mkabaji na mshambuliaji mmoja

Winga Mofosse Tresor Karidioula kutoka klabu ya Haras El Hodood ya Misri anatajwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Simba katika dirisha hili

Beki wa kushoto Khadim Diaw kutoka klabu ya Al Hilal ya Sudan nae tayari amemalizana na Simba kama ilivyo kwa kiungo mkabaji Alassane Kante kutoka klabu ya CA Bizertin ya Tunisia

Lakini pia yumo winga Mohammed Bajaber anayetua Msimbazi akitokea klabu ya Polisi ya Kenya huku pia mshambuliaji Jonathan Sowah akitajwa tayari kamalizana na Simba akitokea klabu ya Singida Black Stars

Mlinda lango Yacoub Mohamed kutoka klabu ya JKT Tanzania anaongoza wachezaji wa ndani ambao tayari wamemalizana na Simba kama ilivyo kwa beki wa kati Wilson Nangu ambaye pia anatokea JKT Tanzania

Kiungo kutoka Coastal Union Hussein Semfuko nae ametajwa kuwa tayari amemalizana na Wekundu hao wa Msimbazi

Tetesi bado zinaihusisha Simba na nyota kadhaa wa kigeni na ndani kama kiungo wa Zoman Fc, Privat Djessan Bi, Feisal Salum - Azam Fc, Yahya Zayd - Azam Fc, Abdallah Kulandana - Fountain Gate na mshambuliaji Dramane Kamagate anayeitumikia San Pedro ya Ivory Coast

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema wamekamilisha usajili wa nyota wote waliowahitaji katika dirisha hili lakini zoezi la usajili litafungwa baada ya kumalizika michuano ya CHAN 2024 itakayoanza kutimua vumbi August 02 hadi Augut 30 katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania

Ahmed alisema watatumia michuano hiyo kumalizia nafasi chache ambazo wataziacha mahsusi wakiamini kuna nafasi ya kupata wachezaji bora katika michuano hiyo

Semaji ametamba kuwa Simba itakapoanza kutambulisha wachezaji, wengine wote watakaa kimya kwa mshtuko watakao-kutana nao


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.