Local,Normal News,Simba

Simba kufanya pre-season Misri

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Jul 2025
Simba kufanya pre-season Misri

Baada ya majadiliano ya ndani na tathmini ya kina, hatimaye klabu ya Simba imechagua Misri kuwa ngome ya maandalizi ya msimu ujao wa mashindano 2025-2026 ikiwa ni mkakati wa kujenga kikosi madhubuti kitakachopambana kwa ajili mataji ndani na nje ya nchi, huku siri ya kutimkia huko ikitajwa.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka klabu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi, kikosi kinatarajiwa kuondoka Jumatano ya wiki ijayo kuelekea moja kwa moja kwenye mji wa Ismailia ambao umewahi kuwa mwenyeji wa mechi za AFCON na kambi za timu mbalimbali barani Afrika kutokana na mazingira yake rafiki.

Simba imekuwa kwenye mjadala wa ndani kwa wiki kadhaa kuhusu wapi pa kuweka kambi, ikiwa na mapendekezo makubwa mawili mezani kutoka kwenye benchi lao la ufundi ambapo ni Misri au Uturuki.

Ingawa Uturuki ilikuwa chaguo lenye mvuto wa kimataifa na miundombinu ya hali ya juu, gharama na uhusiano wa karibu wa Simba na baadhi ya vituo vya mafunzo nchini Misri ulifanya uchaguzi kuwa mwepesi. Ikumbukwe kuwa msimu uliopita pia kikosi hicho kiliweka kambi eneo hilo.

"Kulikuwa na tathmini ya kina. Kocha Fadlu Davids na benchi lake waliweka vigezo kadhaa kwanza, mazingira ya hali ya hewa, pili ufanisi wa mazoezi, na tatu ukaribu wa kijiografia. Misri ikawa chaguo bora kwa vigezo vyote hivyo," chanzo cha ndani kutoka Simba kilinukuliwa na Mwanaspoti.

Ismailia ni mji uliopo kando ya Mfereji wa Suez, wenye miundombinu ya kisasa ya michezo, hoteli bora, na viwanja vya mazoezi vya daraja la kwanza.

Pia una hali ya hewa ya joto ya wastani ambayo ni rafiki kwa maandalizi ya kimwili, hasa kwa timu kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.

Hii ni mara nyingine tena Simba inakwenda Misri kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya ikiwa na matumaini ya kufanya vizuri 2025-2026.

Msimu uliopita 2024-2025, Simba ilijichimbia katika mji wa Ismailia nchini Misri ikiwa chini ya Kocha Fadlu Davids.

Kabla ya hapo, Simba maandalizi ya msimu wa 2023-2024 ilipokuwa ikinolewa na Roberto Oliveira 'Robertinho' ilikwenda Uturuki, huku msimu wa 2022-2023 kambi yao ikiwa mji wa Ismailia nchini Misri wakati kocha akiwa Zoran Maki.

Tayari baadhi ya wachezaji wa ndani wanajifua Mo Simba Arena huku nyota wa kigeni wakiwemo wapya waliosajiliwa wakitua nchini kuanzia siku ya Jumamosi

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
48m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’