Simba kuweka kambi ya maandalizi Misri

Joel JJ By Joel JJ β€’ 29th July 2025


Simba kuweka kambi ya maandalizi Misri

Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka nchini kesho Jumatano kuelekea Misri kuanza maandalizi ya msimu mpya wa mashindano, 2025/26

Taarifa iliyotolewa na Simba mapema leo, imebainisha kuwa timu itaondoka Alfajiri, kambi hiyo ikitarajiwa kuwa mji wa Ismailia

Wachezaji wapya wanaungana na wenzao wanaoitumikia Simba tangu msimu uliopita kuelekea katika kambi hiyo

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema nyota pekee watakaokosekana katika kambi hiyo ni wale walio katika majukumu ya timu za Taifa kushiriki michuano ya CHAN inayoanza mwishoni mwa wiki

Simba inatarajiwa kuhitimisha kambi yake August 28 na kurejea nchini tayari kwa msimu mpya wa mashindano mbalimbali


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.