Tanzania iko tayari kwa ufunguzi CHAN 2024

Joel JJ By Joel JJ β€’ 31st July 2025


Tanzania iko tayari kwa ufunguzi CHAN 2024

Jumamosi August 02 2025 timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itaweka karata yake ya kwanza katika michuano ya CHAN 2024 itakapoikaribisha Burkina Faso katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashiriki katika nchi za Tanzania Bara, Zanzibar, Kenya na Uganda

Tanzania imepewa heshima ya kipekee kwani uzinduzi wa michuano hiyo utafanyika hapa nchini

Ni wazi CAF wameichagua Tanzania kuzindua michuano hiyo kutokana na hamasa ya mashabiki, Tanzania imejipambanua kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi viwanjani

Tiketi zinaendelea kuuzwa hivyo kama hujakata tiketi yako, bado una siku mbili. Hili ni jambo letu kama Watanzania, hivyo tujitokeze kwa wingi kuiunga mkono timu yetu ya Taifa

Tanzania ni moja ya timu zinazopewa nafasi ya kufanya vizuri katika michuano hii kutokana na ubora wa kikosi chake

INAWEZEKANA kombe hili likabaki hapa Tanzania, kwa umoja, ushirikiano na sapoti ya Watanzania wote, INAWEZEKANA


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.