Yanga yashusha mshambuliaji Mcongomani

Joel JJ By Joel JJ • 1st August 2025


Yanga yashusha mshambuliaji Mcongomani

Jana usiku Yanga ilitambulisha usajili wa mshambuliaji Andy Boyeli raia wa DR Congo aliyekuwa akiitumikia klabu ya Sekhukhune ya Afrika Kusini

Kocha Mpya wa Yanga Romain Folz ndiye aliyependekeza usajili wa mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita aliifunga  Sekhukhune mabao saba ligi kuu ya Afrika Kusini 

Msimu wa 2022/23 Boyeli aliitumikia Power Dynamos ya Zambia ambapo alitwaa kiatu cha mfungaji bora baada ya kufunga mabao 18 huku akitwaa tuzo ya MVP

Boyeli ndiye mrithi wa Kennedy Musonda aliyetimkia Israel baada ya mkataba wake kumalizika


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.