International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumamosi, August 02 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 Aug 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumamosi, August 02 2025

Tottenham, Manchester United na Newcastle wanamfuatilia mshambuliaji wa Paris St-Germain Randal Kolo Muani, 26, baada ya uhamisho wa mchezaji kwenda Juventus kukwama. (Le Parisien)

Winga wa Manchester United Muargentina Alejandro Garnacho, 21, bado ana nia ya kutaka kuhamia Chelsea wakati akijaribu kuondoka Old Trafford msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)

Jaribio la Chelsea la kutaka kumsajili mshambuliaji wa RB Leipzig Mholanzi Xavi Simons, 22, limegonga mwamba kwani timu hiyo ya Bundesliga haitaki mchezaji yeyote wa kikosi cha klabu hiyo ya Premier League kwa kubadilishana (Sun)

Valencia wanakaribia kumpa mkataba mpya kiungo wa kati wa Uhispania Javi Guerra, 22, ambaye anaivutia Manchester United na AC Milan. (Marca)

West Ham wamewasilisha dau la euro 8m (Β£6.9m) kwa mlinda lango wa Botafogo Mbrazil John Victor, 29, wakati Galatasaray, Everton na Manchester United hapo awali walionesha nia. (Fabrizio Romano)

Lyon wako kwenye mazungumzo na Liverpool kuhusu uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Tyler Morton, 22. (Sky Sports)

Manchester City wako tayari kuwauza kiungo wa kati wa Uingereza Jack Grealish, 29, James McAtee, 22, na Kalvin Phillips, 29, pamoja na mlinda lango wa Ujerumani Stefan Ortega, 32, msimu huu wa joto, mradi tu watapata ofa zinazofaa. (Athletic)

Beki wa kushoto wa AZ Alkmaar David Moller Wolfe, 23, anasafiri kwenda Uingereza kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika klabu ya Wolves, huku raia huyo wa Norway akitarajiwa kununuliwa kwa pauni milioni 12. (Sky Sports)

Beki wa Inter Milan,Yann Bisseck, 24, amekataa uhamisho wa kwenda Crystal Palace, ambao dau la pauni milioni 28 lilikubaliwa kwa Mjerumani huyo. (Gazzetta dello Sport)

Atalanta wamekataa dau la pauni milioni 36.5 kutoka kwa Inter kwa winga wa Nigeria Ademola Lookman huku wakitaka kitita cha pauni milioni 43.5 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Fabrizio Romano)

Middlesbrough wamekubali dili la thamani ya Β£3.5m kumnunua beki wa kulia wa Blackburn Muingereza Callum Brittain, 27. (Sky Sports).

BBC

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
5h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
9h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
11h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
13h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
15h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
15h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
16h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
18h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
21h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’