Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imeanza vyema kampeni ya kuwania taji la michuano ya CHAN 2024 ikiichapa Burkina Faso mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Stars ilitawala mchezo huo pengine kama safu ya ushambuliaji wangekuwa makini, mabao zaidi yangefungwa
Bao la kwanza lilipatikana kupitia mkwaju wa penati baada ya Clement Mzize kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari
Abdul Suleiman Sopu alitumia vyema pigo hilo la penalti kuiandikia Stars bao la uongozi likiwa ni bao la kwanza katika michuano hiyo
Kipindi cha pili Stars iliendelea kutawala mchezo na kufanikiwa kuongeza bao la pili kupitia kwa Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' aliyemalizia krosi ya Idd Nado ndani ya eneo la hatari
Ni ushindi muhimu ambao unafuta rekodi mbaya ya Tanzania kutopata ushindi katika michuano hiyo hii ikiwa mara ya tatu kushiriki

