Yanga yaweka malengo mapya 2025/26

Joel JJ By Joel JJ β€’ 4th August 2025


Yanga yaweka malengo mapya 2025/26

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amewataka wachezaji wa timu hiyo kusahau mafanikio waliyopata msimu uliopita na kuwekeza nguvu ili kufanya vyema zaidi msimu ujao 2025/26

Akizungumza katika semina iliyofanyika jijini Dar es salaam jana ambayo iliwakutanisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi, Hersi alisema mafanikio yote ya msimu uliopita yameingia kwenye historia na sasa kila kitu kinaanza upya

"Hii ni familia imara sana, familia hii imekuwa na mafaniko makubwa katika misimu minne iliyopita, tunashukuru kwa mafanikio hayo tuliyopata lakini niwahakikishie yote yamekuwa historia"

"Tunaachana na historia sasa tuna kazi ya kufanya. ni msimu mpya na wote tunaanza tukiwa kwenye mstari mmoja"

"Iwe timu iliyonusurika kushuka daraja msimu uliopita au mabingwa, wote tunaanza katika mstari mmoja"

"Tusahau yote tuliyofanya msimu uliopita, mabao tuliyofunga, asisti au idadi ya mechi tulizoshinda yote yamekuwa historia. sasa tunakwenda kukabiliana na msimu mpya," alisema Hersi

Kikosi cha Yanga kimeanza rasmi maandalizi yake kujiandaa na mikiki mikiki ya 2025/26 ambapo kocha Romain Folz atakuwa na takribani siku 10 za kujiandaa kabla ya mechi yake ya kwanza y pre-season dhidi ya Rayon Sports itakayopigwa August 15 huko Rwanda


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.