Local,Normal News,Yanga, Simba, Azam, Fountain Gate, Singida BS

Morocco aitabiria makubwa Stars CHAN 2024

Joel JJ By Joel JJ
5 Aug 2025
Morocco aitabiria makubwa Stars CHAN 2024

Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burkina Faso, juzi usiku kwenye mchezo wa ufunguzi wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka kwenye ligi za ndani ya nchi zao (CHAN), Kocha Mkuu wa Tanzania, Taifa Stars, Hemed Suleiman 'Morocco', amesema walichokiona Watanzania ni kidogo tu, kwani watarajie makubwa kwenye kikosi hicho, akitamba kufanya vyema katika michezo ijayo.

Akizungumza mara baada ya ushindi wa kihistoria, Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo kwa mara ya kwanza nchi ikiwa mwenyeji wa mashindano hayo ya nane yaliyoanza kufanyika mara ya kwanza 2009 nchini Ivory Coast, Morocco, alisema anaiona Stars imekuwa na kikosi bora zaidi kuliko wakati mwingine wowote, hivyo hakuna sababu ya kutofanya vyema kwenye michuano hii.

"Tunashukuru vijana wetu wamejaribu kufanya kile ambacho tumekifanyia kazi, ingawa bado haijawa vile ambavyo tunahitaji”

“Nafikiri tumeanza vizuri na lengo letu lilikuwa ni hilo, tutajaribu kila hali kuhakikisha tunakuwa bora kila baada ya mechi"

“Ilikuwa mechi ya presha sana kwa sababu ndiyo ya kwanza, mechi ya ufunguzi tunacheza nyumbani mbele ya mashabiki wetu, tulihitaji zaidi ushindi ili tujiweke kwenye nafasi nzuri ya msimamo na kuwatia moyo mashabiki wetu, isingekuwa vyema sisi ni wenyeji, halafu mechi ya kwanza mnafungwa, tunaamini mechi zilizofuata tutakuwa bora zaidi kuliko leo"

“Tuna kikosi bora kwa sasa kuliko wakati mwingine wowote ule na hilo nalisema mapema, tutahakikisha tunafanya vizuri zaidi kuliko miaka mingine ya nyuma, hii ndiyo kwanza tumeanza," alitamba Morocco.

Kocha huyo alisema wakati wanakwenda maandalizi walijua mapungufu yao na eneo ambalo wana ubora, hivyo wakafanyia kazi maeneo ambayo wana matatizo.

"Wakati tunaanza maandalizi tulijua timu yetu haina wastani mzuri wa kufunga mabao, ila tulijua tuna safu nzuri ya ulinzi kwa maana hiyo tulifanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa tunazitumia vizuri nafasi," alisema.

Stars itarejea tena uwanjani Jumatano saa 2:00 usiku, kucheza mchezo wa pili wa Kundi B, dhidi ya Mauritania. Kundi hilo pia lina timu za Afrika ya Kati na Madagascar ambalo kituo chake ni Dar es salaam, kikicheza Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha shilingi milioni 40 kwa Stars, baada ya ushindi huo.

Akizungumza na wachezaji wa timu hiyo wakati akiwakabidhi fedha hizo, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paramagamba Kabudi alisema Rais amefurahishwa sana na matokeo hayo.

"Rais amefurahishwa na kazi nzuri mliyoifanya leo fedha hizi ni ahadi ambayo aliitoa kwa ajili ya kuwapa motisha naamini mtaendeleza ushindani huu kwenye michezo ijayo," alisema Kabudi.

Mbali na fedha hizo vile vile alitoa shilingi milioni 20 kama zawadi kutoka Wizara yake, na kudai analipongeza benchi la ufundi la timu hiyo kwani limeipa fahari Taifa.

Alisema ni wakati wa kupambana ili wachukue ubingwa wa michuano hiyo ambayo ushindani na upinzani mkubwa. Aidha aliwashukuru Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu hiyo ilipokuwa inapambana.

Alisema serikali imefanya maandalizi makubwa ili kuona Tanzania inapata ubingwa wa mashindano hayo. Michuano hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano wa nchi tatu za Afrika Mashariki, Tanzania, Kenya na Uganda.

IPP Media

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE →
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE →
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE →
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE →
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE →
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE →
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE →