International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne August 05 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 Aug 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne August 05 2025

Mshambuliaji wa Slovenia kutoka RB Leipzig, Benjamin Sesko (22), anatumia mbinu za kisiasa katika usajili kwa kuzitumia Newcastle na Manchester United kuzipambanisha ili apate dili bora zaidi.

Newcastle wameonyesha nia mpya ya kumsajili beki wa kati wa England, Marc Guehi, kwa ofa ya takriban pauni milioni 40, lakini Crystal Palace wanataka pauni milioni 50 ili kumuachia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.

Kocha David Moyes anataka kufanya usajili wa hadi wachezaji sita zaidi kwa ajili ya Everton, ikiwa ni pamoja na viungo wa kati wawili na wachezaji wa pembeni wawili. Tottenham wameambiwa watalazimika kulipa euro milioni 30 (pauni milioni 26) ili kumsajili kiungo wa Hispania Marc Casado (21) kutoka Barcelona.

Winga wa Brazil Rodrygo (24) anataka kubaki Real Madrid licha ya kuvutiwa na Tottenham, Arsenal na Liverpool.

Crystal Palace wanakabiliana na ushindani kutoka Juventus katika harakati za kumsajili beki wa kulia wa Girona, Arnau Martinez (22) raia wa Hispania.

Kiungo wa kati wa Napoli na Sweden, Jens Cajuste (25), anapendelea kurejea Ipswich Town kuliko kwenda Burnley au ligi ya Saudi Arabia. Stuttgart wanakaribia kufanikisha dili la kumsajili kiungo wa kati wa Ureno, Fabio Vieira (25), kutoka Arsenal.

Porto walivutiwa na beki wa Poland Jakub Kiwior (25), lakini walikataa kutimiza thamani ya euro milioni 30 (pauni milioni 26) iliyowekwa na Arsenal.

Tottenham wanatataka kumuuza kiungo wa kati kutoka Mali, Yves Bissouma (28), ili kutoa nafasi kwa Conor Gallagher, kiungo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 25 kutoka Atletico Madrid.

Liverpool wanafuatilia maendeleo ya beki wa Brentford na timu ya taifa ya Ireland, Nathan Collins (24). West Ham wamewasilisha ofa mpya ya pauni milioni 10 kwa Botafogo ili kumsajili kipa wa Kibrazil John Victor (29).

Bayer Leverkusen wanamtaka mshambuliaji wa Denmark wa Manchester United, Rasmus Hojlund (22), lakini wanakumbana na ushindani kutoka AC Milan, Inter Milan na Juventus.

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’