Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wamepania kuendeleza mafanikio katika soka la ndani na zaidi kufanya vyema zaidi katika michuano ya ligi ya mabingwa (CAF CL) msimu ujao
Kamwe ametamba kuwa pesa nyingi zimetumika katika dirisha hili la usajili ili kuleta wachezaji ambao watatimiza mipango ya Yanga katika michuano hiyo ya ligi ya mabingwa
"Ninauhakika wa zaidi ya Asilimia 80 msimu unaokuja sio tu kwenye ligi ya ndani, Yanga itakuwa tishio hadi kwenye ligi ya mabingwa (CAF CL)".
"Mwaka uliopita hatukufanya vizuri kwenye Champions League, tulitoka hatua ya makundi na hiyo ndio ikamtia hasira Rais wetu wa Klabu Injinia Hersi Said akaenda kufanya usajili mkubwa"
"Nyote mlimsikia akisema kwamba usajili wa mwaka huu ndio usajili bora kuliko miaka yake yote minne aliyofanya usajili kwenye timu hii"
"Hajawadanganya, amefanya usajili bora, usajili ambao umetumia hela nyingi kuhakikisha msimu unaokuja tukirudi kwenye Champions League haturudi kinyonge, tunarudi tukiwa wazito, wakubwa na wenye uwezo wa kufanya makubwa, " alisema Kamwe katika uzinduzi wa kampeni ya kuchangia tofali la ubingwa, Geita
Yanga tayari imeanza maandalizi ya msimu ujao, wakijifua katika uwanja wa KMC Complex chini ya kocha mkuu Romain Folz



