Droo ya mechi za hatua ya awali na raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAF CL) imefanyika leo jijini Dar es salaam ambapo Simba imepangwa kuchuana na Gaborone United ya Botswana katika hatua ya awali
Mchezo wa kwanza utapigwa Botwana na mechi ya marudiano kupigwa wiki moja baadae jijini Dar es salaam
Aidha kama Simba itafanikiwa kutinga raundi ya kwanza, itachuana na mshindi wa mchezo kati ya Simba Bhora ya Zimbabwe dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Malawi
Katika mchezo wa raundi ya kwanza Simba pia itaanzia ugenini na kumalizia nyumbani
Mechi za raundi ya awali zitapigwa Septemba 19-21 leg 1 na Septemba 26-28 leg 2