Local,Normal News,Simba

Fadlu afunguka mikakati ya kuikabili Gaborone United

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Aug 2025
Fadlu afunguka mikakati ya kuikabili Gaborone United

Kocha Mkuu wa Simba Fadu Davids amesema wamepokea droo ya hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na sasa wanafanya maandalizi kabambe ili kuhakikisha wanafuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika katika ngazi ya klabu

Droo ya mechi za hatua ya awali na raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAF CL) ilifanyika juzi jijini Dar es salaam ambapo Simba ilipangwa kuchuana na Gaborone United ya Botswana katika hatua ya awali

Mchezo wa kwanza utapigwa Botwana na mechi ya marudiano kupigwa wiki moja baadae jijini Dar es salaam

Aidha kama Simba itafanikiwa kutinga raundi ya kwanza, itachuana na mshindi wa mchezo kati ya Simba Bhora ya Zimbabwe dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Malawi

Fadlu amesema Gaborone United sio timu nyepesi lakini anafurahi kwa kuwa kikosi chake kitacheza mechi ya kwanza Botswana na kumaliza mechi ya pili uwanja wa Benjamin Mkapa

"Tunajua ligi ya mabingwa ni mashindano makubwa zaidi kuliko kombe la Shirikisho tulilocheza msimu uliopita ambalo tulianza hatua ya awali dhidi ya timu ngumu ya Al Ahly Tripoli, wakati huu tunaanza na Gaborone United"

"Tunajua haitakuwa mechi nyepesi, najua ni timu yenye wachezaji wapambanaji na wagumu wanapocheza katika uwanja wao wa nyumbani"

"Lakini sisi tunaamini katika uwezo wetu, msimu huu tumeunda timu imara zaidi ambayo inaweza kupambana katika mazingira magumu, pia tuna uzoefu baada ya ushiriki wetu michuano ya kombe la Shirikisho msimu uliopita"

"Timu yetu imeimarika zaidi na niseme tu, tuko tayari kwa michuano hii ya ligi ya mabingwa msimu huu"

"Tutafanya tathmini ya kina kabla ya kukabiliana nao, tayari tunawafahamu Jwaneng Galaxy, Township Rollers na hata hawa Gaborone United ni timu zenye uzoefu na mashindano haya"

"Tutapambana ili kuhakikisha tunavuka raundi hii," alisema Fadlu

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
7h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
11h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
14h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
16h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
17h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
17h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
19h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
23h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’