Local,Normal News,Yanga

Nyota wapya Yanga waanza kutema cheche

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Aug 2025
Nyota wapya Yanga waanza kutema cheche

Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports uliopigwa uwanja wa Amahoro huko Rwanda, aliwaanzisha wachezaji wanne wapya

Viungo Moussa Balla Conte, Mohamed Doumbia winga Celestin Ecua na mshambuliaji Andy Boyeli walianza kipindi cha kwanza katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1

Ukiwa ni mchezo wa kwanza wa ushindani tangu Yanga ilipoanza kujifua siku 10 zilizopita, nyota hao walionyesha umahiri wao na kuwapa matumaini mashabiki wa Yanga juu ya ubora wa timu yao siku za usoni

Conte alishirikiana vyema na safu ya ulinzi kwa kukata umeme huku Doumbia akionekana kila mahali eneo la kiungo akiichezesha timu

Ecua alionyesha hatari yake ndani ya eneo la hatari, kulikuwa na matukio ya winga huyo aliyetua kutoka Asec kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari lakini mwamuzi hakuchukua hatua

Dakika 45 alizotumika katika mchezo huo zilimtosha Boyeli kuonyesha Yanga haikukosea kumfuata Afrika Kusini

Boyeli alifunga bao la kusawazisha la Yanga kabla ya kutengeneza bao la pili liililofungwa na Pacome Zouzoua

Baada ya mapumziko, Folz aliwatoa nyota hao akifanya mabadiliko ya karibu kikosi kizima nyota wengine wapya Lassine Kouma, Offen Chikola na Edmund John nao wakipata nafasi

Chikola alikuwa kivutio zaidi dakika 45 za kipindi cha pili akihusika katika bao la tatu lililofungwa na nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto

Mpira wake wa kona ulitendewa haki na Mwamnyeto aliyeujaza mpira kimiani kwa kichwa na kuihakikishia Yanga taji la kwanza katika pre-season

Akizungumza baada ya mchezo huo, Folz alisema bado timu yake haijapata muunganiko lakini anawapongeza wachezaji wake kwa kutimiza angalau kwa asilimia chache ya kile walichokiandaa

"Tumekuwa na bahati mbaya kuruhusu goli la mapema ambalo ni uzembe pia muda mwingi tuliachia mipira kizembe, bado hatujazoeana kiufundi na kimbinu, niseme wazi bado tuko mbali na kile tunachokitaka," alisema Folz

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’