Simba leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wadi Degla inayoshiriki ligi kuu ya Misri
Ni mchezo wa nne wa kirafiki kwa Simba ambayo inahitimisha pre-season hapo kesho
Mabao ya Simba yalipatikana katika kipindi cha pili yakifungwa na Elie Mpanzu aliyefunga bao la kuonga kwa shuti la mbali kabla ya Kibu Denis kuongeza bao la pili akimalizia krosi ya Jean Charles Ahoua
Katika mchezo huo Mkufunzi wa Simba Fadlu Davids alianza na Camara, Chasambi, Naby Camara, Caraboua, Rushine, Morice, Maema, Ahoua, Mukwala, Kibu na Mpanzu
Vijana wa Fadlu leo walitawala mchezo na pengine wangeweza kuondoka na ushindi wa mabao matatu kama bao la Steven Mukwala lisingekataliwa ikiwa offside




