Local,Normal News,Yanga

Yanga wamkumbuka Mzee Katundu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Aug 2025
Yanga wamkumbuka Mzee Katundu

Leo imekuwa siku ya kipekee kwa familia kubwa ya Yanga SC, baada ya Rais wa Klabu, Injinia Hersi Said, kumtembelea Katibu wa zamani wa Yanga, Mzee Jabir Katundu, na kumkabidhi zawadi za jezi mpya za msimu wa 2025/26.

Mzee Katundu, ambaye aliwahi kuhudumu kama Katibu wa Klabu kati ya mwaka 1962 hadi 1966, alihudumu chini ya Uenyekiti wa marehemu Mohamed Mabosti. Kipindi chake cha uongozi kilikuwa cha kihistoria, kwani kilisaidia kuimarisha msingi wa Yanga na kuiweka kwenye ramani ya soka la Tanzania na Afrika Mashariki.

Katika ziara hiyo, Rais Hersi Said alikabidhi kwa heshima kubwa jezi zote tatu za matoleo mapya ya msimu huu, huku akimuelezea Mzee Katundu dhamira na maudhui yaliyopelekea ubunifu wa jezi hizo.

Kila jezi inabeba simulizi na alama ya heshima kwa historia na mafanikio ya klabu, zikionyesha mshikamano kati ya vizazi vilivyopita na kizazi cha sasa.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
6h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
10h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
11h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
13h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
16h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
16h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
16h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
18h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
22h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’