Local,Normal News,

Singida BS kujinoa Kagame Cup

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Aug 2025
Singida BS kujinoa Kagame Cup

Kocha Mkuu wa Singida Black Stars, Miguel Gamondi amesema mashindano ya Kagame yatamsaidia kuandaa timu shindani kuelekea mechi za ligi na kimataifa.

Akizungumza na Mwanaspoti, Gamondi alisema anafurahishwa na mwenendo wa maandalizi huku akidai kuwa wachezaji wake wapo kwenye hali nzuri ya ushindani matarajio yao ni makubwa.

β€œTimu inaendelea vizuri licha ya kwamba sio wachezaji wote wapo kikosini wanaendelea kuungana nasi kidodo kidogo lakini matarajio ni makubwa na wachezaji wengi wapo tayari kwa ushindani,” alisema na kuongeza:

β€œNahitaji kuwa na kikosi chote kambini ili kuwa na machaguo sahihi. Nafikiri siku zinavyozidi kwenda wachezaji wengi wanawasili na nafikiri mashindano haya ambayo tumepata nafasi ya kushiriki yatatoa mwanga mzuri kwetu.”

Gamondi alisema ni nafasi sahihi kwao kushiriki michuano hiyo baada ya kufanya mazoezi kwa muda na kukosa mechi za kirafiki zilizo na hadhi ya ushindani, hivyo wanaamini michuano hiyo itawapa nafasi ya kufanya kitu sahihi na kutambua ubora na udhaifu.

β€œNi michuano mizuri inakutanisha timu nyingi, hivyo tutapata mechi nyingi ambazo zitaongeza utimamu kwa wachezaji ukiondoa mazoezi ya kuchezea mipira uwanjani tunahitaji mechi nyepesi na ngumu ili kujua upungufu na ubora wetu,” alisema.

Gamondi alisema wamejiandaa na mikakati ni kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michuano hiyo ili kuwapa mwanga mzuri wapi wanaanzia kimataifa na ligi ya ndani.

β€œTuna timu nzuri ambayo imesheheni vipaji vikubwa na uzoefu... nafikiri hili litathibitishwa kwenye uwanja wa mashindano na naamini tutapata maandalizi mazuri kupitia mashindano hayo ambayo yanatarajia kuanza mapema mwezi ujao.”

Gamondi amejiunga na Singida Black Stars baada ya kuiongoza Yanga kwa misimu miwili akiipa mataji ya ndani na kuifikisha timu hiyo hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’