Mshambuliaji Clement Mzize amechagua kuendelea kutumikia Yanga baada ya kuongeza mkataba
Baada ya majadiliano ya wiki kadhaa hatimaye Yanga imeshinda, ikifanikiwa kumbakisha mshambuliaji wake muhimu
Yanga ilipokea ofa nyingi kwa ajili ya Mzize katika dirisha hili, Esperance ya Tunisia ikitajwa kuwasilisha ofa nono zaidi inayofikia dola Milioni 1
Yanga iliweka iliweka wazi mpango wa kumbakisha mshambuliaji huyo ambaye aliiongoza Taifa Stars katika michuano ya CHAN akifunga mabao mwili
Mzize ataendelea kusalia Yanga hadi mwaka 2028



