Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids ameeleza kuridhishwa na mwenendo wa kikosi chake baada ya wiki nne za pre-season huko Misri
Leo Simba inakamilisha mechi ya mwisho ya kirafiki dhidi ya FS Fassel ya Liberia kabla ya kurejea Tanzania siku ya kesho Alhamisi
Akizungumza jana baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wadi Degla, Fadlu alibainisha kuhitaji kuongezewa mshambuliaji mwingine ambaye ataendana na ushindani wa mechi kubwa za maamuzi
"Niwe tu muwazi bado nahitaji mchezaji mmoja mwenye X Factor kwenye eneo la ushambuluaji, najua tumepata sapoti kubwa sana kutoka kwa Rais Mo Dewji na mchango wake msimu huu umekuwa mkubwa Sana"
"Natumai sasa tunapoelekea mwishoni mwa usajili Jayrutty anaweza kutusaidia kumpata mchezaji huyo mmoja mkubwa ambaye anaweza kutupa utofauti kwenye eneo la mwisho"
"Unakumbuka baadhi ya mechi ngumu msimu uliopita tulikuwa tunakosa mchezaji mkubwa ambaye anaweza kukupa hizo x Factor, mechi kama ya fainali ya CAF CC na hata mechi ya mwisho wa msimu dhidi ya Yanga tulikuwa tunakosa mchezaji kama huyo"
"Tunahitaji kufanya vyema kwenye ligi ya ndani lakini pia tunakazi kubwa ya kufanya kimataifa,β alisema Fadlu katika mahojiano ya Azam TV
Simba imerejesha nchini mshambuliaji Seleman Mwalimu aliyekuwa akiitumikia Wydad CA, inaelezwa tayari usajili wake umekamilika na atajiunga na kikosi jijini Dar es salaam